1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyota ya Leipzig yaendelea kuangaza

7 Novemba 2016

Vijana wapya wa Bundesliga RB Leipzig wanashikilia usukani wa ligi kwa pamoja na Bayern Munich wakiwa na pointi 24 kila mmoja. Leipzig waliwacharaza Mainz 3-1 katika mpambano ambao wangefunga mabao mengi zaidi.

Fußball Bundesliga Timo Werner RB Leipzig Mainz  Red Bull Arena GER 1 BL 10
Picha: Imago/Picture Point LE

Vijana hao ambao sasa wametoshana na Bayern kwa kushinda mechi saba na kutoka sare tatu baada ya mechi zao kumi msimu huu, wameifikia rekodi ya timu inayocheza msimu wake wa kwanza katika Bundesliga, iliyowekwa na MSV Duisburg, ambayo pia ilicheza mechi kumi bila kushindwa katika msimu wa 1993/94. 

Ulikuwa mpambano wa kawaida wa timu mbili zilizofanyiwa mabadiliko, ulikuwa mgumu sana, lakini tulikuwa katika hali ya juu kutokana na ukweli kwamba tulifunga mabao matatu. Lakini kama haufungi bao la nne au la tano, basi mpinzani hupata motisha, lakini muhimu ni kuwa ulikuwa mchuano wenye mafunzo na ulikuwa mchezo ulioonyesha ukomavu.

Schalke ilipata ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Werder Bremen. Schalke sasa hawajashindwa katika mechi tisa na sasa wamepanda katika nafasi ya 12 kutoka nafasi za mkia. Bremen sasa imetumbukia katika eneo hatari la kushushwa daraja. Alessandro Scöpf ni kiungo wa Schalke ambaye pia alifunga bao moja

Bayern hawaonekani kuwa imara chini ya mfumo wa kocha Carlo AncelottiPicha: picture-alliance/nordphoto/Straubmeier

Lazima tuseme kuwa sasa tuna pointi 11 baada ya mech 10. Hizo sio nyingi sana. Kila wakati tunafikiria kuhusu kucheza mechi na kuendelea kutia bidii katika mechi zijazo ili kupata pointi tatu ikiwezekana. Siku ya jumamosi, Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mabao manne wakati Borussia Dortmund iliwabamiza washika mkia Hamburg mabao 5-2. BVB sasa wako katika nafasi ya tano

Mjini Munich, Bayern walinyimwa ushindi wao wa sita mfululizo na nambari tatu kwenye ligi Hoffenheim, ambayo wamehifadhi rekoidi yao ya kutoshindwa mchuano kufikia sasa katika ligi msimu huu. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 matokeo ambayo yalimridhisha kocha wa Hoffenheim Julian Nagelsmann

Mwishowe tuna furaha kuwa hatukufungwa bao la pili na tumeridhika kabisa na matokeo. Sio rahisi kuwa hatujashindwa hadi sasa. Hivyo tukiangalia tunakotoka, ni maendeleo mazuri, na tunataka kuendelea hivyo.

Bayer Leverkusen ilipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Darmstadt, wakati Wolfsburg ilisonga hadi nafasi ya 14 kutokana na ushindi wa 3-0 dhidi ya Freiburg, ushindi wao wa kwanza tangu msimu ulianza. Augsburg iliishinda Ingolstadt 2-0 wakati Cologne ikishuka hadi nafasi ya sita kwenye ligi baada ya kichapo cha moja bila na Eintracht Frankfurt.

Studioni niko na mwenzangu Sekione Kitojo kuzungumzia Bundesliga, Kitojo, suali ambalo watu wanajiuliza ni je, Lepzig wanaweza kuwaangusha Bayern na kutwaa taji la Bundesliga?

Mwandishi:_Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW