Nyumba za wanasiasa wa upinzani zimeshambuliwa Burundi
21 Agosti 2007Matangazo
Kisa hicho kimetokea mjini Bujumbura na kuhusisha mwanasiasa mmoja wa chama tawala na naibu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani FRODEBU. Polisi wanaendelea na uchunguzi japo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. Wakati huo huo wabunge 69 waliwasilisha barua kwa Rais Perre Nkurunziza na kutoa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Chama tawala nchini humo CNDD-FDD kinakabiliwa na mvutano wa kisiasa baada ya mwenyekiti wake maarufu Hussein Rajabu kuondolewa kwa madai ya kusababisha vurugu.
Mwandishi wetu Amida Issa anaripoti zaidi kutoka Bujumbura.