Obama akutana na wanajeshi Kabul
20 Julai 2008Matangazo
Seneta Barack Obama alizungumza nao juu ya maarifa yao waliopata nchini Afghanistan-nchi ambayo imejionea hivi karibuni kuzidi kwa machafuko mwaka huu.
Obama akiwa pamoja na ujumbe wa wabunge wa Marekani wa Baraza la congress,amepanga kuonana pia na Rais Hamid Karzai baadae hii leo-kwa muujibu wizara ya nje ya afghanistan ilivyoarifu.
Ziara hii ya Bw.Obama nchi za nje tangu kuteuliwa mtetezi wa kiti cha urais,itamchukua pia Iraq,Jordan,Israel,Ujerumani,Ufaransa na mwishoe Uingereza.
Madhumuni ya ziara hii ya Bw.Obama ni kukuza kipaji chake cha maarifa ya siasa za nje na kuwajibu wakosoaji wake wanaodai hana maarifa ya kuwa amirijeshi-mkuu.