1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

270110 Obama Rede

28 Januari 2010

Rais wa Marekani Barack Obama amelihutubia bunge la nchi yake kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.Hotuba yake ilijikita katika masuala ya kuuimarisha uchumi,kuunda nafasi mpya za kazi

Rais Barack Obama akilihutubia Bunge Capitol Hill ,WashingtonPicha: AP

Hata hivyo mapendekezo yake ya kuubadili mfumo mzima katika sekta ya afya bado yamekwama.Pindi baada ya ukumbi kufunguliwa rasmi, Rais Obama alianza moja kwa moja kuielezea hoja yake muhimu ya kuuimarisha uchumi.Kiongozi huyo alikiri kuwa anayafahamu malalamiko na wasiwasi wa raia wa Marekani ukiuzingatia uhaba wa nafasi za kazi na hali ya kiuchumi.Rais Obama alitoa wito wa kuyatoza ada maalum mabenki makubwa,''Napendekeza mabenki makubwa yatozwe ada maalum.Ikiwa mashirika haya yanaweza kutoa bakshishi kubwa ina maana yanaweza kuzilipa fedha zilizotumiwa kuyaokoa yaliypokuwa yanayumbayumba.''alisema.

Kupigwa jeki

Wabunge wakisikiliza hotuba ya Rais Obama kwa makiniPicha: AP

Rais Obama aliingia madarakani yapata mwaka mmoja uliopita wakati ambapo nchi yake ilikuwa imegubikwa na matatizo makubwa ya kiuchumi aliyoyarithi.Ili kuwapa moyo raia wake Rais Obama alikiri kuwa anafahamu kwamba wanakabiliwa na kipindi kigumu hivyo basi wanahitaji kupigwa jeki,''Napendekeza tutumie kiasi cha dola bilioni 30 zilizorejeshwa na mabenki makubwa kuyaimarisha mabenki madogo ili yaweze kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo ndipo biashara zistawi.''alisistiza.


Kubadili mtazamo

Kuhusu suala la kufanya mageuzi katika mfumo mzima wa afya, Rais Obama aliibadili kauli yake kwa kusema kuwa hajakata tamaa na akalitolea wito bunge kutowasahau raia wa kawaida.Pembezoni mwa harakati zote hizo za kuwapa moyo raia wa Marekani,Rais Obama alimpongeza pia mke wake Michele Obama anayeandaa mpango mpya wa kuwahamasishia watoto umuhimu wa afya bora,''Ningependa pia kumtambua mama wa taifa Michele Obama anayeanzisha mpango maalum wa kuwahamasisha watoto kuwa na afya nzuri hususan kupunguza uzito wa mwili.Msimtazame sana…..ana haya jamani!...''

Rais Obama na mkewe Michelle mwaka mmoja uliopita baada ya kuapishwaPicha: AP

Wiki mbili zilizopita Rais Obama nusura afanikiwe katika mapendekezo yake ya kuubaduili mfumo wa afya.Ushindi wa mwanachama wa Republik katika jimbo la Massachusetts iliyo ngome ya chama tawala cha Demokratik nao pia umeibadili sura ya chama cha Rais Obama.Rais Obama aliugusia umuhimu wa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na matumizi ya nishati mbadala.Hata hivyo alilikwepa suala nyeti la kuvipunguza viwango vya gesi za viwanda katika mazingira zinazoaminika kuchangia katika ongezeko la joto ulimwenguni.

Akiihitimisha hotuba yake iliyodumu zaidi ya saa zima Rais Obama alilitolea wito bunge kuwa imara.''Kamwe hatutotikisika.Tuchukue nafasi hii kuwa na mwanzo mpya,kutimiza ndoto yetu ili tuuimarishe muungano wetu.Ahsante na Mungu awabariki.''

Mwandishi:Thelma Mwadzaya-ZPR-Bergmann ,C

Mhariri:Liongo Aboubakary

Audio-Link:

ENDE

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW