1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama anaanza ziara yake Afrika

Oumilkher Hamidou26 Juni 2013

Rais Barack Obama anaanza ziara yake ya pili rasmi barani Afrika kama rais wa Marekani (26.06.2013). Ataanzia ziara hiyo nchini Senegal, kabla ya kwenda Afrika Kusini na kumalizia Tanzania.

U.S. President Barack Obama (L) and First Lady Michelle wave as they board Air Force One to depart from Berlin June 19, 2013. Obama's first presidential visit to Berlin comes nearly 50 years to the day after John F. Kennedy landed in a divided Berlin at the height of the Cold War and told encircled westerners in the city "Ich bin ein Berliner", a powerful signal that America would stand by them. REUTERS/Thomas Peter (GERMANY - Tags: POLITICS)
Obama BerlinPicha: Reuters

Maratajio yalikuwa makubwa barani humo alipochaguliwa rais huyo mwenye asili ya kiafrika kuwa rais mwaka 2008. Nani kama si yeye ambae angetoa kipaumbele kwa bara la Afrika? Mhula wake wa pili ulipoanza matarajio hayo kidogo yamepwaya.Juhudi zake kuwelekea Afrika zinaonyesha hafifu zikilinganishwa na zile za mtanagulizi wake.

"Nna daamu ya kiafrika mwilini mwangu na historia ya familia yangu mwenyewe inachanganya tangu misiba mpaka mafanikio ya historia ya bara la Afrika." Hayo ndiyo matamshi aliyochagua kuyatamka rais Barack Obama aliefanya ziara fupi nchini Ghana mwaka 2009.

Furaha na shangwe zilikuwa kubwa alipotaja asili yake ya kiafrika. Kwamba wakati huo huo alilaani rushwa barani Afrika na kushinikiza watu wawajibike, hayo watu waliyafumbia masikio. Nani kama si rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya kiafrika, atakaefungua ukurasa mpya wa sera ya marekani kuelekea Afrika, kuhimiza vitega uchumi vya moja kwa moja na kuinua shughuli za utalii?

Rais Obama na familia yake walipokaribishwa Ghana 11-07-2009Picha: AFP/Getty Images

Hali lakini imejitokeza vyengine: Migogoro iliyoathiri sekta ya nyumba na  uchumi nchini Marekani ilimlazimisha rais Obama anaesalitika zaidi na siasa ya ndani, atangulize mbele masilahi ya kijiografia na kulilenga zaidi  bara la Asia na wakati huo huo kuelekeza mawazo yake katika bara la Afrika .

Kauli za wasomi kuhusu ziara hiyo

Professor David Shinn aliyewahi kuwa balozi wa Marekani nchini Ethiopia na Burkina Faso na ambae hivi sasa ni mhadhiri wa siasa za kimataifa katika chuo kikuu cha George Washington anachambua siasa ya Marekani kuelekea Afrika kwa kusema:" Ni kweli kwamba awamu ya kwanza ya utawala wa Obama haikutoa umuhimu mkubwa sana kwa bara la Afrika. Bila ya shaka watu walijiwekea matumaini makubwa.Lakini majukumu muhimu ya siasa ya ndani yalizuka na kufanya iwe shida kushughulikia kwa nguvu masuala ya Afrika.Hilo atalisawazisha katika awamu yake hii ya pili.Ndio maana safari hii ameanza mapema safari hii ndefu".

Hata hivyo si sawa kuwasingizia Obama na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani kwamba hawajishughulishi na masuala ya Afrika. Katika mzozo wa Sudan, Obama aliingiliaa binafsi au aliwatuma wajumbe wake maalum ili kuhakikisha kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan kusini inafanyika kama ilivyopangwa mwaka 2011. Mwaka uliofuatia viongozi wa Afrika walifunga safari hadi Camp David kutokana na mwaliko wa rais Obama, kuhudhuria mkutano wa kundi la mataifa manane tajiri kiviwanda uliopitisha azimio kuhusu mkakati wa kudhamini "usalama wa chakula" duniani.

Mkakati huo unaendelezwa katika nchi 20 zikiwemo Senegal na Tanzania. Hata hatua zinazozusha mabishano zimechukuliwa na serikali ya rais Obama:kwa mfano walipotuma vikosi maalum vya Marekani katika Afrika kati ili kumsaka mkuu wa waasi wa LRA Joseph Kony,au walipoanzisha ujenzi wa vituo vya ndege zinazorzushwa bila ya rubani nchini Athiopia,Niger na Djibuti.

Mwandishi:Ludger Schadomsky/Feleke,Abebe/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Yusuf Saumu

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW