Obama Sieg
7 Novemba 2012Sera ya fedha zimesaidia kuitowa Marekani katika msukosuko na kuepusha msukosuko wa pili wa kiuchumi. Hata kabla ya kutimiza mwezi mmoja madarakani baada ya kuchaguliwa, Obama alisaini mpango wa wa uokozi wa dola bilioni 787. Miongoni mwa sera alizoendelea nazo ni pamoja na kuyaokoa mabenki . Hali ya kiuchumi si nzuri bado, huku ukosefu wa ajira ukiwa kiawango cha nane asili mia na hivyo bado ni cha juu. Lakini pamoja na hayo waataalamu wanakiri kwamba bila ya hatua hizo hali ingekuwa mbaya zaidi.
Moja wapo ya changamoto kubwa zinazomkabili Obama katika kipindi hiki cha pili ni deni kubwa la dola trilioni 16. Rais huyo ametoa wito wa hatua za mchanganyiko wa ongezeko la kodi na kupunguza matumizi, ambazo kimantiki ndiyo njia pekee ya kujitowa katika mgogoro wa madeni.
Sera ya kijamii
Katika sera ya jamii, hivi sasa mpango huo unaweza kuanza kazi kisheria baada ya kutetewa na Obama kwa jitihada kubwa. Muhula wa pili una maana sasa mamilioni ya Wamarekani wanaweza kupata bima ya afya na halitokuwa jambo la kuwamaliza kifedha pindi wanapoumwa. Mitt Romney alitishia kuachana na mpango huo wa Obama.
Mafanikio mengine ya Obama
Obama anaweza kutaja mafanikio yake katika masuala mengine ya kisheria kama kuhakikisha wanawake wanapata mishahara sawa na wanaume na pia suala la mashoga kutumika jeshini. Kwa hivyo inachukuliwa kuwa Rais alifuata sera za kibinaadamu, mahala ambapo Warepublican walipinga. Hivyo makundi ya wachache katika jamii nayo kupewa nafasi ya kutowa mchango wao katika ujenzi wa uchumi wan chi hiyo.
Sera ya nje
Katika sera ya kigeni, kusita kwake katika masuala ya Iran na Syria si jambo linaloeleweka, lakini huenda amechukuwa msimamo huo kutokana na ahadi aliyotoa 2008 kwamba atajaribu kusafisha sura ya Marekani na kuondoa hisia za chuki dhidi ya taifa hilo, na badala yake kuwa mshirika. Hatua ya kimataifa nchini Libya ni mfano mzuri wa mafanikio yake. Urais katika mamlaka ya Mitt Romney , ingekuwa shida kuuelewa msimamo wa Republican takriban katika Nyanja zote. Obama ameweza kutawala miaka mine iliopita kwa busara. Wamarekani wanahitaji mtu wa aina hiyo na kwa kuwepo Barack Obama, wameweza kumchaguwa mtu wa aina hiyo.