1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama kuhutubia mkutano mkuu wa chama cha Democratic

21 Agosti 2024

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amerudi katika jukwaa la kitaifa usiku wa kuamkia leo ili kumuunga mkono mwandani wake katika chama cha Democratic Kamala Harris.

Marekani | Mkutano wa  chama cha Kidemokrasia
Rais Barack Obama, akiwa jukwaani na mkewe Michelle wakati wa Kongamano la Kitaifa la chama chake cha Democratic (DNC) huko Chicago, Illinois, Marekani, Agosti 20, 2024Picha: Alyssa Pointer/REUTERS

Hilo ni katika azma yake ya dakika za mwisho ya kuwania urais dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump. Muda mfupi ujao Obama atauhutubia mkutano huo mkuu wa chama cha Democratic ila kabla hapo, mkewe Michelle ambaye Wademocrat wengi walikuwa wanampigia debe kuchukua nafasi ya Biden katika kuwania urais, atatoa hotuba yake pia. Kulingana na chanzo kinachofahamu kuhusiana na hotuba ya Obama, rais huyo wa zamani wa Marekani anatarajiwa kuangazia kile anachoamini kwamba, kitamuinua Harris na kumpelekea kupata ushindi ila wakati huo huo pia, atawatahadharisha Wademocrat kuhusiana na kazi ngumu waliyo nayo katika kipindi cha miezi 11 ijayo. Obama mwenye umri wa miaka 63, ana ushawishi mkubwa katika chama cha Democratic na hasa wakati ambapo chama hicho kinapoyumbishwa na migogoro.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW