Obama na Clinton katika mtihani wa kampeini zao
6 Mei 2008Maseneta wawili wa Marekani,Barack Obama na Hillary Clinton leo jumanne wanakabiliwa na mtihani mgumu katika kinga'anyiro chao cha kutaka kuelekea ikulu ya White House. Hii ni kutokana na kuwa wanachama cha Democratic wa majimbo ya Indiana na North Caroline wanapiga kura kutafuta nani kati ya maseneta hao wawili anapendwa zaidi.
Anaeshinda kura hizo atakuwa na uwezo zaidi wa kuweza kuchaguliwa kama mgombea wa kiti cha urais.
Majimbo haya yana umuhimu wake kwa watetezi wote wawili.Yanajumulisha wajumbe 187 wa mkutano mkuu wa Agosti ambao utaamua nani akiwakilshe chama hicho.Kwa hivyo majimbo haya ndio zawadi pekee iliobaki katika kinyang'anyiro ambacho baado ni kikali kwa wote.Baada ya matokeo haya michuano ambayo itakuwa imesalia itakuwa sita tu.
Kabla ya siku ya leo watahiniwa wawili, Obama na Clinton, kila moja amekuwa akidai kuwa yeye ndie ataibuka na ushindi wa kura za leo.Akiwahutubia wafuasi wake katika kituo cha mafuta cha New Albany Indiana usiku wa kuamkia leo alisema kuwa mchuano ni wa kufa na kupona na kuwaomba watafakari zaidi,huku akiwapa moyo akisema chama chake kingekuwa na sheria kama za Republican angekuwa kwa sasa amukuwa amesha teuliwa.
Ushindi wa Hillary Clinton katika majimbo yote mawili unaweza ukavunja nguvu za uwezo wa Obama na hivyo kushawishi baadhi ya wajumbe wakuu wa chama,walio na uamuzi wa mwisho,kumugeukia yeye.
Lakini mpinzani wake, Barack Obama si kidogo kwani anaongoza imani ya wajumbe wa chama watakaokuwa na jukumu la nani apamabane na seneta MacCain.Ingawa Clinton alimshinda katika uchaguzi wa jimbo la Pennsylvania mwezi jana lakini hakuvunjwa moyo.
Endapo Obama atashinda majimbo yote mawili katika uchaguzi wa jumanne,bila shaka ndoto ya Bi.Hillary Clinton ya kuendelea kumuongoza mpinzani wake katika kura za wajumbe pamoja na kura za wananchi katika majimbo yote itakuwa imefifia.Pia huenda kushindwa kwa Clinton,ikiwa kutatokea,kunaweza kukaongeza miito ya kumtaka akae kando na kumwachia Obama aendele na kazi.
Lakini kati ya wote wawili hakuna anaeweza kupata uungwaji mkono wa wajumbe unaotosha kabla ya kumalizika kwa uchaguzi wa Juni 3,kuweza kuwachia wajumbe wakuu takriban 800 kuweza kufanya kazi hiyo.
Ikiwa wote watagawana kura sawa,itamaanisha kuwa hali itabaki ileile hadi chaguzi zilizosalia sita ambazo zinawajumbe 217.
Obama amekuwa akipambana katika kampeini zake kufuatia kushindwa mwezi jana.Pia kampeini zimezongwa na matamshi yanayosemwa kuwa hayakuwa mazuri kwa wakazi wa mta mmoja katika jimbo la Pennsylvania na pia uhusiano wake na mchungaji mtatanishi Jeremiah Wright.
Obama ikiwa atashinda yote haya, atakuwa rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika alisema jumatatu kuwa yaliyompata siku chache zilizopita yamemtakasa.