1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama na wapiga kura Waislamu.

Kitojo, Sekione25 Julai 2008

Barack Obama anaweza kutegemea uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa kutoka kwa jamii ya Waislamu nchini Marekani katika uchaguzi wa mwezi Novemba lakini kuna hatari ya kuwaudhi.

Mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani kwa tikiti ya chama cha Democratic Barack Obama akisali katika eneo la wayahudi wakati alipofanya ziara mjini Jerusalem hivi karibuni.Picha: AP



Barack Obama anaweza kutegemea uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa kutoka kwa Waislamu nchini Marekani katika uchaguzi wa mwezi Novemba, iwapo maoni ya wapigakura yako sahihi, lakini kuna hatari ya kuwaudhi baadhi ya waumini wa imani hiyo kutokana na kujieleza kuwa yeye si mmoja wao.


Idadi ya kura ni ndogo kwa kuwa Waislamu ni sehemu ndogo tu ya idadi ya watu nchi Marekani na hakuna hesabu za kuaminika juu ya ni wangapi wamejiandikisha kupiga kura.

Lakini kwa historia ya sasa ya uchaguzi wa rais wenye ushindani mkubwa , hakuna kura ambayo inaweza kupuuziwa wakati Obama kutoka chama cha Democratic , ambaye huenda akawa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika , anapambana dhidi ya mgombea wa chama cha Republican John McCain.

Uchunguzi uliofanywa na pew Forum kuhusu dini na siasa umegundua kuwa asilimia 63 ya Waislamu nchini Marekani ama wanajihesabu kuwa ni wafuasi wa chama cha Democratic ama wanaelemea katika mwelekeo huo, ikilinganishwa na asilimia 11 ambao wanasema kuwa wanaunga mkono chama cha Republican ama wanajitambulisha karibu na chama hicho.

Wakati huo huo , kiasi cha asilimia 12 ya Wamarekani wanafikiri kuwa Obama ni Muislamu, dhana ambayo imeendelea kuwapo kwa miezi kadha na imeingizwa kama uvumi katika mtandao wa Internet.

Suala ambalo hilo linalogusa lilikuwa katika habari tena wakati gazeti la New Yorker lilipochapisha picha ya kuchekesha ya kuchora katika ukurasa wake wa mbele inayomwonyesha Obama akiwa amevaa nguo za Kiarabu na mkewe akiwa na bunduki katika ikulu ya Marekani na bendera ya nchi hiyo ikiwa inungua katika jiko la kuleta joto. Kumekuwa na ripoti pia ambazo hazijathibitishwa kuwa kampeni ya Obama inapanga kuteua watu watakaowasiliana na jamii ya waislamu. Sehemu ya masuala ya dini katika wavuti ya Obama , pambana na upakaji matope, ambayo iliundwa kupambana na uvumi kama huo, unaompakazia madai kuwa ni Muislamu, kuwa ni uongo na kueleza kuwa hajawahi kuwa Muislamu, hajakuzwa kama muislamu na yeye ni muumini halisi Mkristo.

Tunafahamu kuwa si Muislamu, lakini nani anajali hilo ,iwapo ni Muslamu, amesema Sofian Zakkout , mkurugenzi wa chama cha Wamarekani Waislamu katika Marekani ya kaskazini.

Ahadi ya Obama kuzileta pamoja jamii, ndio kinachomvutia , Zakkout amesema, na hatumtarajii kuja kwetu na kusema niko nanyi. hatuhitaji hilo.

Lakini Saaqib Rangoonwala , mkurugenzi mtendaji wa Infocus ambalo ni gazeti la Kiislamu katika eneo la kusini la Califonia, anaona kuwa huu utakuwa uchaguzi ambao wagombea watakuwa karibu mno katika kura ambapo kura za Waislamu wa Marekani zitahitajika na ni wakati ambao Waislamu lazima wachukua msimamo.

Waislamu hawamshughulishi sana Obama kuliko makundi mengine , na amekutana na kiongozi wa Waislamu na binafsi aliomba radhi kwa wanawake wa kiislamu ambao walipigwa marufuku na wahusika wa kampeni yake kukaa nyuma ya jukwaa katika mkutano wa kampeni wa Detroit kwasababu wanawake hao walikuwa wamevaa hijabu.

Ahmed Rehab, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya baraza la mahusiano ya Waislamu nchini Marekani mjini Chicago, amesema kuwa kuna kiwango cha juu cha hamasa katika uchaguzi wa rais miongoni mwa Waislamu, suala kuu likiwa haki za raia, amani katika mashariki ya kati, uhamiaji, uchumi na chuki dhidi ya Waislamu.


►◄




Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW