1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama sasa anaelekea kumteua Hillary Clinton kuwa waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Marekani

Eric Kalume Ponda21 Novemba 2008

Kamati kuu inayoisuka serikali ya Rais Mteule Barrak Obama nchini Marekani, inasema kuwa rais huyo mteule , sasa inaelekea kumteua Hillary Rodham Clinton, mke wa Rais wa zamani Bill Clinton.

Hillary Clinton huenda akateuliwa waziri wa mambo ya nchi za nje katika serikali ya Barrak Obama.Picha: AP


Kamati kuu inayohusika na kuisuka serikali ya Rais Mteule Barrak Obama nchini Marekani, inasema kuwa rais huyo mteule , sasa inaelekea kumteua Hillary Rodham Clinton, mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinto katika wadhifa wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo.

Wasaidizi wa karibu kwenye kundi hilo linaloisuka serikali ya Barrak Obama, itakayoapishwa Januari 20 mwakani, wanasema kuwa mipango ya kumteua Hillary Clinton imepiga hatua kubwa baada ya kupigwa jeki na rais wa zamani Bill Clinton◄


Baada ya kukutana wiki iliyopita na kufanya mazungumzo ya muda mrefu huko Chicago, Rais huyo mteule Barrak Obama, anaonekana kumjongelea zaidi Hillary Clinton ambaye alikuwa mpinzani wake wakati wa kampeini ya uteuzi wa mgombea urais wa chama cha Demokrati.


Punde tu baada ya mashauriano hayo, imebainika kwamba Barrak Obama anadhamiria kumteua Hillary Clinton katika wadhifa wa warizi wa mambo ya Nje nchini Marekani kuchukua mahala mwa Condolizza Rice.


Msimamo huo ambao imekuwa ikienezwa na vyombo vya habari kama uvumi tu, huenda ukatimia wiki ijayo, wakati rais huyo mteule anapotarajiwa kumteua Hillary, mke wa rais wa zamani nchini Marekani Bill Clinton baada ya sherehe za chama cha Demokrat Novemba 27, kusherehekea ushindi wa Barrak Obama.


Ingawa Clinton hajatangaza hadharani iwapo atakubali uteuzi huo, ishara ziko wazi kwamba sasa Hillary Clinton anaelekea kuchukua wadhifa huo, baada ya mumewe Bill Clinton kutangaza kwamba atachunguza upya,kuimarisha na kupanua shughuli za wakfu wake wa Bill Clinton iwapo mkewe atateuliwa katika wadhifa huo.

Duru zinaasema kuwa pande hizo mbili zimekuwa zikifanya mazungumzo tangu siku ya Jumatatu wiki hii, kutafuta njia za kuimarisha ufadhili kwa wakfu huo wa Bill Clinton unaoendesha shughuli zake katika jumla ya mataifa 27.


Wakati huo huo waziri wa ulinzi nchini Marekani Roberts Gate, amekutana na kamati andalizi kuhusu masuala ya usalama katika serikali ijayo ya Barrak Obama, na kuongeza uvumi kwamba huenda Robert Gates akasalia katika wadhifa huo katika serikali mpya ijayo ya Barrak Obama.


Gate alikutana na maafisa wakuu wa kamati hiyo ya Barrak Obama, John White na Michele Flournoy, na msemaji katika makao makuu ya wizara ya Ulinzi Geoff Morrel.


Huu ulikuwa mkutano wa kwanza baina ya waziri huyo wa ulinzi na kamati hiyo andalizi ya rais mteule Barrak Obama, ambapo kamati hiyo, pia katika hali ya kujiandaa, inatarajiwa kuchunguza maongozi, utaratibu wa utendaji kazi katika idara hiyo, kwa ushirikiano na waziri huyo wa ulinzi.


Uvumi kuhusu uteuzi wa Robert Gates katika wadhifa huo, ulianza kuenea baada ya mshauri mkuu wa Barrak Obama kuhusu maongozi ya kigeni, Richard Danzig, kusema kuwa Robert Gates anauzoefu katika kazi hiyo na ingekuwa vyama kuhudumu katika serikali ya Barrak Obama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW