1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ofisi ya Chadema Arusha yachomwa moto usiku

14 Agosti 2020

Watu wasiojulikana wanadiwa kuvamia na kuchoma moto jengo la ofisi ya chama kikuu cha upinzania Chadema kanda ya kaskazini zilizopo Arusha Tanzania, na kusababisha uharibifu wa mali ambazo thamani yake haijajulikana.

Tansania Angriff auf Büro von Chadema in Arusha
Picha: DW/V. Natalis

Hayo yanajiri wakati ambapo yamebaki masaa machache kwa mgombea urais kupitia chama hicho kuwasili katika ofisi hizo kwaajili ya zoezi la kutafuta wadhamini jeshi la polisi limesema linafanya msako mkali kuwabaini waliohusika.

Mapema asubuhi ya leo katika ofisi hizi za Chadema kanda ya kaskazini wafuasi wa chama hicho, walikusanyika kushuhudia tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo. Inaelezwa kuwa watu wasiojulikana walivamia ofisi hizo na kumpiga mlinzi na baadae kutekeleza tukio la kuchoma moto ofisi hizo.

Sehemu ya nje ya ofisi ya Chadema ilivyogeuka baada ya tukio la kuchomwa moto usiku wa kuamkia Ijumaa, Agosti, 14, 2020.Picha: DW/V. Natalis

 Reginald Masawe ni katibu wa chama cha Chadema mkoa wa Arusha amesema walipata taarifa saa tisa usiku kwamba ofisi zao zimevamiwa. Ofisi hizo zinahusisha ofisi za kanda ya kaskazini, ni ofisi pia za Chadema mkoa wa Arusha, na pia ni ofisi za Chademawilaya.

Soma pia Wananchi wa Arusha wajitokeza kwa wingi kupiga kura

"Kwahiyo usiku huo huo nilipopata taarifa nilifika hapa na kukuta kuna uharibifu mkubwa, mlinzi tulimkuta hali yake sio nzuri kwa sababu ukiangalia nyuma mgongoni amepigwa sana. Ukiangalia kwenye mikono alikua amefungwa Kamba kwahiyo mikono imechubuka na kwenye miguu,” ameongeza kusema.

Polisi yaombwa kuchunguza kwa kina

Wafuasi wa chama hicho wanasema suala hilo linatishia usalama wao wa kidemokrasia mahali ambapo mchakato wa uchaguzi mkuu unaendelea kwa sasa katik ataifa hilo la Afrika mashariki huku wakiliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina.

"Hili tukio kwakwali kwa mimi mwanachama wa kawaida, nalihusisha na mambo ya kisiasa kwakua Lissu anakuja leo, wanajaribu kuharibu mapokezi yake kama mgombea urais.”

"Kwakweli hili tukio la ofisi ya chama kuungua moto sio jambo zuru,ni jambo la kulaaniwa na kila mtanzania lakini Mungu wetu ni mwaninifu na Mungu atatusaidia.”

Kamanda wa polisi kanda ya Arusha ACP Salum Hamduni, akizungumza na waandishi habari kuhusu tukio la kuchomwa moto ofisi ya Chadema mkaoni Arusha, Ijumaa, Agosti 14, 2020.Picha: DW/V. Natalis

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Salumu Hamduni amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi hilo linafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote waliohusika.

"Katika kata ya Kimandolu tarafa ya Suye katika halmashauri ya jiji la Arusha ofisi ya chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kanda ya kaskazini ,ilichomwa moto na kuteketeza baadhi ya samani ambazo ni viti vya mbapo pamoja na mito yake.

Unaweza kusoma pia CHADEMA yapinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa Monduli-Arusha

Nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wananchi na wakazi wote wa Arusha kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kutupatia taarifa, na tungefurahi zaidi watupe taarifa sahihi, ili tuweze kuwakatama na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,” amesem Kamanda Hamduni.

Chanzo: Veronica Natalis DW ARUSHA.