1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oktoba mosi: Siku ya Kimataifa ya wazee duniani

1 Oktoba 2021

Oktoba mosi dunia inaungana pamoja kuadhimisha siku ya wazee duniani na kauli mbiu mwaka huu ni usawa wa matumizi ya kidijitali kwa wote. Nia haswa ni kutoa ufahamu kuhusu changamoto wanazopitia wazee

alte Frau arbeitet auf dem Feld
Picha: picture-alliance/blickwinkel/Blinkcatcher

Kauli mbiu mwaka huu ni usawa wa matumizi ya kidijitali kwa wote, inayomaanisha umuhimu wa kufikiwa na kushirikishwa kikamilifu kwa wazee katika masuala ya kidijitali.

mapinduzi ya viwanda ambayo yametawaliwa na uvumbuzi mkubwa sana wa kidijitali na ukuaji uliopo katika sekta hiyo yamebadilisha sekta zote katika jamii ikiwemo namna tunavyoishi kufanya kazi na namna tunavyoingiliana na watu wengine. 

Teknolojia inatoa matumaini ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu.  Lakini ripoti za utafiti za hivi karibuni zinaonesha kwamba wanawake na wazee hawapati nafasi sawa yanapohusika  masuala ya kidijitali. Hawafikii teknolojia ziliopo na hawafaidiki kikamilifu kwa nafasi zilizoko.

Umoja wa Mataifa unasema siku hii ya wazee mwaka huu iinapaswa kutumiwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwahusisha wazee katika huduma za kidijitali. Sera mahususi ziwepo ili wazee wafikishiwe huduma hizo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka 2050 idadi jumla ya watu wazee duniani kuanzia miaka 60 na zaidi itaongezeka na kufikia bilioni 2 kutoka milioni 900 mwaka 2015. K wa sasa watu milioni 125 ni wazee kuanzia umri wa miaka 80 kwenda juu.

Janga la corona limewaathiri wazee kwa kiwango kikubwa

Bibi mzee akipokea chanjo ya COVID 19Picha: Jelena Djukic Pejic/DW

Wakati maisha marefu kwa wazee wetu inamaanisha nafasi kubwa zaidi kwao wao kufanya shughuli mbali mbali, kwa mfano kuwa na kazi mpya japokuwa ndogo na kuchangia shughuli za kijamii, wapo katika hatari ya kukabiliana na magonjwa na ulemavu na kupoteza thamani ya maisha.

Huku dunia bado ikiwa inapambana na janga la corona wazee ni miongoni mwa watu walioathirika pakubwa  kwa kulazimika kubakia nyumbani kwa muda mrefu na hii, kwa baadhi imewaathiri afya zao za akili na hata kutokwenda mara kwa mara kuangalia afya yao kumewafanya baadhi yao kukutwa na hali mbaya za kiafya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wazee ni lazima wapewe kipaumbe katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19.

Amesema ni lazima watu waangalie namna wanavyowashughulikia wazee katika kipindi hiki kigumu na ni muhimu kuimarisha maisha ya wazee katika jamii pamoja na kusikiliza matakwa yao pamoja na kuheshimu haki zao.

Chanzo: Umoja wa Mataifa