1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Ujerumani imempoteza mwanasiasa mweye shauku

27 Desemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Ujerumani imempoteza mwanasiasa mwenye shauku na mdemokrati thabiti,baada ya familia ya waziri wa zamani wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble kutangaza kifo cha kiongozi huyo.

Berlin, Ujerumani | Waziri wa zamani wa fedha Ujerumani Wolfgang Schäuble
Waziri wa zamani wa fedha Ujerumani Wolfgang SchäublePicha: Christian Thiel/imago

Katika taarifa yake, Kansela Scholz amesema upendo wa Schäuble wa mijadala ya kidemokrasia, mtazamo wake wa kihafidhina wa ulimwengu na matamshi yake makali yalimfanya aonekane bora kwa muda mrefu.  

Soma pia:

Wolfgang Schaeuble alitoa mchango mkubwa katika majadiliano ya kuungana upya Ujerumani mbili, ya Mashariki na Magharibi mwaka 1990, na kama waziri wa fedha wakati wa utawala wa Kansela Angela Merkel, alikuwa kiungo muhimu katika juhudi za kubana matumizi zilizosaidia kuiondoa Ulaya katika mgogoro wa madeni zaidi ya miongo miwili baadae.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW