1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olimpiki ya walemavu yaanza rasmi

29 Agosti 2024

Mji mkuu wa Ufaransa Paris ulikuwa mwenyeji hapo jana usiku wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya wanariadha wanaoishi na ulemavu.

Frankreich | Paris2024 | Eröffnungszeremonie der Paralympics in Paris
Picha: Zac Goodwin/empics/picture alliance

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer pamoja na watu kadhaa maarufu.

Jumla ya wanariadha 4,400 kutoka mataifa 168 walishuka kwenye barabara inayopakana na mtaa maarufu wa Champs-Elysees mbele ya maelfu ya watazamaji wanaokadiriwa kufikia 50,000.

Wanariadha wenye ulemavu wa kimwili, viungo kama macho na hata matatizo ya kiakili watashindana katika jumla ya michezo 22 kuanzia leo Alhamisi hadi Septemba 8 mwaka huu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW