OLSZTYN:Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani W Schäuble atoa mwito juu ya kuleta uelewano baina ya Ujerumani na Poland
1 Oktoba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani bwana Wofgang Schäuble ametoa mwito juu ya kuwepo ulewano baina ya Poland na Ujerumani kufuatia hali ya mvutano ya hivi karibuni baina ya nchi mbili hizo.
Waziri Schäuble anaefanya ziara nchini Poland amesema matukio ya vita kuu vya pili asilani yasipewe mwanya wa kujenga mvutano mpya baina ya nchi hizo jirani.
Uhusiano baina ya Ujerumani na Poland umekuwa wa mutano kutokana na kufunguliwa kituo kinachokumbusha juu ya kutimuliwa kwa wajerumani nchini Poland.