1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OMBI LA ARGENTINA LAKATALIWA:

13 Novemba 2003

LONDON: Uingereza imeamua kutoliitikia ombi la Argentina la kumpeleka Argentina mwanadiplomasia wa zamani wa Kiiran.Serikali ya Argentina inamtuhumu Soleimanpour kuhusika na shambulio la bomu lililofanywa mwaka 1994 nchini Argentina dhidi ya Kituo cha Utamaduni cha Kiyahudi.Katika shambulio hilo watu 85 waliuawa.Msemaji wa wizara ya ndani ya Uingereza amesema Argentina hadi hivi sasa haijatoa ushahidi wa kutosha kwa mashtaka yake.Akaongezea kuwa utaratibu wa kumsafirisha mwanadiplomasia huyo wa zamani unaweza kuanzishwa ikiwa Argentina itatoa ushahidi unaohitajiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW