1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ombwe la uongozi DRC linaweza kuwapa nguvu waasi

21 Februari 2024

Wawakilishi wa mashirika ya kiraia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamezungumzia wasiwasi wao kuhusu ombwe la uongozi lililosababishwa na hatua ya kujiuzulu kwa waziri mkuu na mawaziri wengine wengi nchini humo.

DR Kongo | Jeshi la Kongo likipiga doria karibu na eneo la Kibumba, viungwani mwa mji wa Goma
Jeshi la Kongo likipiga doria karibu na eneo la Kibumba, viungwani mwa mji wa GomaPicha: Arlette Bashizi/AFP/Getty Images

Wajumbe hao wamesema hatua hiyo huenda ikatowa mwanya wa kuwapa nguvu waasi na kusambaa kwa machafuko katika eneo hilo.

Jana jioni Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge alipeleka barua yake ya kujiuzulu pamoja na mawaziri kadhaa akiwemo waziri wa ulinzi kwa Rais Felix Tshisekedi katikati mwa machafuko yanayoongezeka. 

Kujiuzulu kwa Kyenge kunafuatia uamuzi wake wa kubakia kuwa mbunge katika bunge la taifa.

Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wameonyesha wasiwasi kufuatia hatua hiyo katika mji wa Goma ambako kuna watu wengi wa wanakimbia kutafuta maeneo yenye usalama.