1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni dhidi ya al Qaeda kuanza Irak

25 Januari 2008
Waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki, amesema vikosi vya usalama vimeanza operesheni muhimu dhidi ya al Qaeda. Akizungumza akiwa mjini Karbala, Al Maliki amesema wanajeshi wa Irak wanaelekea katika mji wa kaskazini wa Mosul kupambana na wanamgambo wa kisunni walio katika ngome yao kubwa ya mwisho. Serikali ya Irak imelilaumu kundi la al Qaeda kwa mlipuko wa mjini Mosul juzi Jumatano uliowaua watu 35.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW