1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

120 wauawa Brazil katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya

30 Oktoba 2025

Zaidi ya watu 120 wameuawa nchini Brazil baada ya polisi kufanya operesheni kabambe ya polisi siku ya Jumatano dhidi ya magenge makubwa ya walanguzi wa dawa za kulevya mjini Rio de Janeiro.

Miili ya waliouawa katika mapambano ya polisi dhidi ya magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya mjini Rio de Janeiro, Brazil
Rio de Janeiro, BrazilPicha: Wagner Meier/Getty Images

Miili ya waliouawa imeshuhudiwa ikiwa imepangwa katika mtaa mmoja usiku wa kuamkia Alhamisi. Taarifa ya polisi imesema mapambano hayo yalilenga kuwafurusha watuhumiwa kuelekea eneo la msitu ambako kikosi maalumu kilikuwa kikisubiri kuwafanyia shambulio la kushtukiza.

Vifo zaidi vinatarajiwa kuongezeka

Idadi ya waliouawa katika purukushani hizo inatarajiwa kuongezeka kwa mujibu wa mamlaka za Rio de Janeiro, Mkuu wa usalama wa mji huo ameahidi kufanya uchunguzi ili kubaini kama polisi walifanya ukiukaji wa aina yoyote wakati wa zoezi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW