Hungary yaionya LGBTQ dhidi ya kuadhimisha siku yao
27 Juni 2025
Maadhimisho haya yanayofanyika katika mji mkuu wa taifa hilo Budapest, licha ya Orban kulipiga marufuku kundi hilo.
Orbnan lakini ametoa onyo kwa waandaaji na washiriki kuhusu matokeo ya kisheria.
Serikali ya muungano inayoogozwa na Orban mapema mwaka huu ilifanyia mabadiliko sheria na katiba ya nchi, kuyapiga marufuku maadhimisho hayo ya kila mwaka, akidai kuwalinda watoto.
Marekani yawaonya raia wake walio ugenini kuhusu uwezekano wa matukio ya LGBTQ kushambuliwa
Wiki iliyopita polisi iliyazuwia maadhimisho hayo ikisema watakaoshiriki watakabiliwa na mkono wa sheria ikidai hatua yake inazuwia kueneza taarifa za LGBTQ kwa watoto walio chini ya miaka 18.
Hata hivyo wandaaji na washiriki wameendelea kusisitiza kuwa mipango yao itaendelea licha ya onyo hilo.