1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Orban: Ukraine kujiuna na Umoja wa Ulaya ni mapema sana

14 Desemba 2023

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán amesisitiza kuhusu msimamo wake kwamba kuanzisha mazungumzo ya Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya itakuwa mapema mno.

Brüssel Umoja wa Ulaya | Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani.Picha: Gaetan Claessens/European Union

Wakati alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kilele wa Umoja huo mjini Brussels hii leo, Orban amewaambia waandishi wa habari kwamba, hakuna sababu ya kuzungumzia uanachama wa Ukraine kwasasana kwamba wameweka masharti saba ya kabla ya mazungumzo na kuongeza kuwa hata kwa tathmini ya Halmashauri kuu ya Umoja huo, masharti matatu kati ya hayo saba hayajatimizwa.

Soma pia:Kuleba apigia debe uanachama wa Ukraine Umoja wa Ulaya

Halmashauri hiyo ilipendekeza kuanza kwa mazungumzo hayo mnamo Novemba, licha ya mapungufu yalioko. Ukraine imekuwa ikirejelea ahadi yake kwamba itatekeleza mageuzi yaliobaki katika muda wa miezi ijayo.

Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya wanaokutana huko Brussels,wanahitajika kuamua kwa kauli mojaiwapo Umoja huo unataka kuanzisha mazungumzo hayo na Ukraine.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW