Wajerumani watatu ni miongoni mwa walioorodheshwa
20 Oktoba 2015Tuzo hiyo ya Ballon d'Or ( mpira wa dhahabu) kwa sasa inashikiliwa na Mreno Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, wamekuwa wakishinda tuzo hiyo kwa miaka saba iliyopita.
Mshambuliaji wa Real Madrid kutoka Wales Gareth Bale ndiye mchezaji Mwingereza pekee aliyetajwa kwenye orodha hiyo.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger ni miongoni mwa makocha 10 wanaowania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka.
Watamenyana na meneja wa Barcelona Luis Enrique aliyeshinda mataji matatu msimu uliopita na kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola.
Katika orodha hiyo, La Liga ya Uhispania inaongoza kwa kuwa na wachezaji 11, nayo Bundesliga ya Ujerumani ina wachezaji sita. Serie A ya Italia ina wachezaji wawili. Ufaransa inawakilishwa na mchezaji mmoja pekee, kigogo wa Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic.
Orodha kamili ya wachezaji:
Sergio Aguero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real Madrid), Karim Benzema (France/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid), Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City), Eden Hazard (Belgium/Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Spain/FC Barcelona), Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona), Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona), Thomas Muller (Germany/FC Bayern Munich), Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich), Neymar (Brazil/FC Barcelona), Paul Pogba (France/Juventus), Ivan Rakitic (Croatia/FC Barcelona), Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich), James Rodriguez (Colombia/Real Madrid), Alexis Sanchez (Chile/Arsenal), Luis Suarez (Uruguay/FC Barcelona), Yaya Toure (Côte d'Ivoire/Manchester City), Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich)
Kocha Bora wa Mwaka Ulimwenguni kwa wanaume:
Massimiliano Allegri (Italy/Juventus), Carlo Ancelotti (Italy/Real Madrid), Laurent Blanc (France/Paris Saint-Germain), Unai Emery (Spain/Sevilla FC), Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich), Luis Enrique (Spain/FC Barcelona), Jose Mourinho (Portugal/Chelsea), Jorge Sampaoli (Argentina/Chilean national team), Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid), Arsene Wenger (France/Arsenal).
Mwandishi: Bruce Amani/AP
Mhariri: Mohammed Abdul-rahman