1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Osama bin Laden kutoa ujumbe kwa nchi za Ulaya

27 Novemba 2007

Kitengo cha kundi la al-Qaeda kimetangaza kitatoa ujumbe mpya hivi karibuni kutoka kwa kiongozi wa kundi hilo, Osama bin Laden.

Bin Laden anatarajiwa kuyalenga mataifa ya Ulaya katika ujumbe wake, lakini hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Tangazo hilo lililoltumwa katika tovuti ya al-Qaeda, lilionyesha picha ya Osama bin Laden akiwa amevalia kanzu nyeupe.

Haijabainika lakini ikiwa ujumbe huo

utatolewa kama ukanda wa video au wa sauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW