Oscar Pistorius kuanza mazoezi mepesi
28 Juni 2013Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Pistorius imesema mwanariadha huyo anayetumia miguu ya kubandikwa ameamua kufanya mazoezi mepesi kwa saa chache kila wikiili kujiandaa kiakili.
Pistorius amesema hatashiriki katika mashindano yoyote mwaka huu wote wa 2013 wakati akikabiliwa na kesi inayooenekana kuchukua muda mrefu ya kumpiga risasi na kumuua Steenkamp, lakini sasa anataka kufanya mazoezi ya mara kwa mara wakati kesi yake ikiendelea.
Kesi yake itaendelea Agosti 19, wakati waendesha mashitaka watakapoamua kama ana mashitaka ya kujibu au la, na tarehe ya kuanza rasmi kesi yake huenda ikawekwa mwezi Septemba au Oktoba. Pistorius mwenye umri wa miaka 26 anakanusha mauwaji ya Steenkamp akisema alimpiga risasi kimakosa kwa sababu alidhani ni mwizi aliyeingia nyumbani kwake. Kama atapatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia, atakabiliwa na adhabu ya kifungo cha chini cha miaka 25 gerezani.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu