1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OSLO: Nchi zataka kupigwa marufuku mabomu mtawanyo

24 Februari 2007

Nchi 46 zilizokuwa zikikutana mjini Oslo Norway zimetia saini makubaliano ya kutafuta mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo ifikapo mwakani.

Uingereza ambayo ni mtumiaji mkuu na pia kuwa na akiba kubwa ya mabomu hayo na Ufaransa ambayo ni mtengenezaji mkuu wa mabomu hayo ni miongoni mwa nchi zilizosaini makubaliano hayo.Japani, Poland na Romania zimekataa kusaini makubaliano hayo wakati mataifa mengine muhimu kama vile Israel,Marekani, China na Urusi hayakushiriki mkutano huo wa Oslo.

Wale wanayoyashutumu mabomu hayo ya mtawanyo wanasema kwamba silaha hizo zinasababisha madhara kwa kiwango kikubwa kisichokukabalika kwa raia.

Makamanda wa kijeshi wanayaona mabomu hayo kuwa silaha yenye ufanisi ambayo huwawezesha kushambulia eneo kubwa kwa pigo moja.

Marekani imesema haitounga mkono kupigwa marufuku kwa matumizi ya silaha hizo.