1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OUAGADOUGOU:Compaore aongoza nchini Burkina Faso

14 Novemba 2005

Uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya jumapili nchini Burkina Faso umemalizika,ikidhaniwa kuwa kiongozi wa sasa Blaise Compaore atarejea madarakani kwa awamu ya tatu kwa mfululizo. Wapinzani wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.Vile vile wamemtuhumu Compaore kuwa ametumia vibaya pesa za serikali,kulipia gharama za kampeni yake ya uchaguzi.Lakini waangalizi wa Umoja wa Afrika wanasema uchaguzi wa safari hii ulikuwa na maendeleo kulinganishwa na chaguzi zilizopita. Matokeo ya uchaguzi hayatarajiwi kutangazwa kabla ya siku ya Alklhamis.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW