1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Padre kujitetea na mauaji ya Rwanda

10 Julai 2005

Arusha:

Padre wa kwanza wa Kikatoliki kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda, Athanase Seromba, ataanza kujitetea mwishoni mwa mwezi wa Oktoba. Kujitetea kwake kumecheleweshwa kwa sababu ya mvutano uliotokea baina ya Mawakili wake. Mawakili wa Padre Seromba wamesema kuwa watawaita Mashahidi kwenye Mahakama hiyo ya Arusha, Tanzania Oktoba 31 ikiwa ni zaidi ya miezi saba baada ya upande wa mshtakiwa kutakiwa ufanye hivyo. Wakili wa Padre Seromba, Patrice Monthe, amesema kuwa atawaita Mashahidi kati ya 25 na 30 kujibu hoja zilizotolewa na Mashahidi 12 wa upande wa mashtaka tokea kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa mwezi wa Septemba mwaka wa jana. Athanase Seromba ni Padre wa kwanza kufikishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya kuhusika na mauaji ya kiholela ingawaje kesi za Mapadre wenzake wawili bado hazijaanza kusikilizwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW