1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan yaihimiza Iran kushirikiana kiusalama

19 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan ametoa wito wa kuwepo ushirikiano wa karibu zaidi katika masuala ya usalama.

Mzozo kati ya Pakistan na Iran
Raia wa Pakistan akionyesha mlima ulioko Koh-e.Sabz huko Pakistan ambako Iran ilifanya shambulizi la angani, Januari 18, 2024 na Pakistan kufanya shambulizi kubwa la kisasi kwenye makambi ya Iran Picha: Banaras Khan/AFP/Getty Images

Wito huo ameutoa leo katika mazungumzo yake ya simu na waziri mwenzake wa Iran, ambapo ameelezea utayari wa Pakistan kushirikiana na Iran katika masuala yote.

Viongozi hao wa mataifa jirani  wamezungumza siku moja baada ya Pakistan kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika kile ilichosema yaliyalenga maeneo ya wanamgambo nchini Iran, kutokana na Iran kufanya mashambulizi wiki hii kuzilenga ngome za wanamgambo nchini Pakistan.

Mazungumzo hayo ya simu yamefanyika baada ya Pakistan kusema haitaki kuzidisha mzozo kati yake na Iran. Hayo yamebainika katika mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu wa kiraia na kijeshi uliofanyika leo kutathmini hali ya usalama baada ya nchi hizo mbili kushambuliana kwa makombora.