1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan kufanya uchaguzi wa mapema mkoa wenye watu wengi

16 Januari 2023

Nchini Pakistan maafisa wamefahamisha kwamba uchaguzi wa mapema utafanyika katika mkoa wenye idadi kubwa ya watu wa Punjab.

Aam Aadmi Party is trying to make a footprint in Bengal
Picha: Payel Samanta/DW

Hatua hii ni baada ya baada ya kiongozi mkuu wa mkoa huo,ambaye ni mshirika wa waziri mkuu wa zamani Imran Khan kuitisha uchaguzi huo na kusababisha shinikizo kubwa kwa serikali mjini Islamabad. Pakistan inajiandaa kuingia kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. Kuitishwa uchaguzi wa mapema katika mkoa wa  Punjab wenye wakaazi milioni 110 ambayo ni takriban nusu ya idadi jumla ya Wapakistan ni hatua ya gharama kubwa kwa serikali ambayo inategemea msaada wa kigeni na inayojikwamua kutokana na athari za mafuriko. Wachambuzi wanasema kwa kusogezwa karibu uchaguzi wa mkoa huo wa Punjab huenda kukaishinikiza serikali kuu kuitisha uchaguzi wa mapema  nchi nzima ili kuepuka gharama ya kufanya uchaguzi mara mbili. Waziri mkuu wa zamani Imran Khan amekuwa akishinikiza uchaguzi wa mapema tangu alipoondolewa madarakani mwezi Aprili mwaka jana kupitia kura ya kutokuwa na imani nae.