1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Pakistan na Sweden zripoti visa vya virusi va homa ya nyani

16 Agosti 2024

Siku moja baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kutangaza kuwa virusi vya homa ya nyani ni dharura ya kiafya duniani, Mataifa ya Pakistan na Sweden yameripoti visa vya kwanza kwenye mataifa yao.

WHO
Shirika la Afya duniani WHO limetangaza kuwa virusi vya homa ya nyani ni dharura ya kiafya duniani.Picha: Denis Balibouse/REUTERS

     
Siku moja baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kutangaza kuwa virusi vya homa ya nyani ni dharura ya kiafya duniani, Mataifa ya Pakistan na Sweden yameripoti visa vya kwanza vya watu wenye virusi vya homa hiyo kwenye mataifa yao. 

Mapema leo siku ya Ijumaa, idara ya afya kaskazini mwa mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa nchini Pakistan imeripoti kesi tatu za wagonjwa wa homa ya virusi ya nyani.Wagonjwa hao walikuwa wamewasili kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu. Hata hivyo hapo kabla wizara ya afya ya nchi hiyo iliesema imebaini mgonjwa mmoja aliambukizwa maradhi hayo. Hadi sasa haijawa wazi iwapo mgonjwa huyo aliyethibitishwa na wizara ya afya ni miongoni mwa hao watatu walioripotiwa hii leo kwenye jimbo la Khyber.

Mgonjwa wa homa ya virusi ya Nyani.Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Soma zaidi. Wagonjwa watatu wa homa ya nyani wagunduliwa Pakistan

Vilevile taarifa ya wizara ya afya ya Pakistan bado haijaweka wazi kuwa mgonjwa huyo alizitembelea nchi gani ya Mashariki ya Kati, Ingawa kwa mujibu wa WHO ni kwamba kumekuwepo na visa 16 vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo katika taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu tangu mwaka 2022.

Kwa sasa maafisa mbalimbali wa afya nchini Pakistan wamepelekwa katika vituo vya mpakani na kwenye viwanja vya ndege ili kuhakikisha ufuatiliaji mkali na kukusanya sampuli kwa vipimo vya afya endapo wataona dalili za ugonjwa kwa abiria wanaorejea kutoka mataifa mengine.

Sweden yaripoti kisa cha kwanza

Kwingineko barani Ulaya,     Sweden imethibitisha kisa cha kwanza cha homa ya virusi ya nyani. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Waziri wa Afya na Masuala ya Kijamii wa Sweden Jakob Forssmed amesema.

Homa ya virusi ya NyaniPicha: Brain WJ/BSIP/picture alliance

"Sasa hivi, sisi pia, mchana wa leo,  tunathibitisha kwamba tuna kesi moja nchini Sweden ya aina mbaya zaidi ya virusi vya homa ya nyani, ile inayoitwa Clade I. Bila shaka, hili ni jambo ambalo tunalichukulia kwa uzito. Wakati huo huo, hii ni kazi ambayo huduma zetu za afya na mashirika ya kuzuia maambukizo ya kikanda wanaweza na wamepanga utaratibu na mifumo ili kushughulikia.''

Soma zaidi.Sweden yatangaza kisa cha kwanza cha virusi hatari zaidi vya mpox 

Katikati mwa wiki hii , Shirika la Afya Duniani WHO lilisema kuwa tayari kuna maambukizi ya watu ya zaidi ya watu 14,000 na vifo 524 barani Afrika mwaka huu pekee, Idadi ambayo tayari imezidi ile ya mwaka uliopita na zaidi ya asilimia 96 ya visa vyote na vifo vimekuwa nchini Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW