1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan, Saudi Arabia zasaini mikataba ya mabilioni ya dola

11 Oktoba 2024

Wafanyabiashara wa Pakistan na Saudi Arabia wamesaini mikataba 27 ya awali kwa ajili ya uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni mbili za Kimarekani

Pakistan Shehbaz Sharif
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif.Picha: K.M. Chaudary/AP/picture alliance

Mikataba hiyo inahusisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, teknolojia, kilimo, madini, afya na nishati.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, na mkuu wa majeshi mwenye ushawishi mkubwa, Jeneralli Asim Munir, walishuhudia sherehe za utiaji saini zilizofanyika jana mjini Islamabad.

Soma zaidi: Wafuasi wa Imran Khan wakabiliana na polisi Islamabad

Sharif alisema kwenye hotuba yake kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha mikataba hiyo inatakelezwa kikamilifu. Sharif aliishukuru Saudi Arabia kwa kuisaidia kupata mkopo wa dola bilioni saba kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Makubaliano hayo yamesainiwa siku moja tu baada ya Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia, Khalid al-Falih, kuwasili nchini Pakistan.

Islamabad imekuwa na uhusiano mzuri na Riyadh, ambayo inaongoza kwa uuzaji mafuta nchini Pakistan. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW