1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Pakistan, Saudi Arabia zasaini ushirikiano wa ulinzi

18 Septemba 2025

Saudi Arabia na Pakistan zimesaini mkataba wa ulinzi wa pamoja ambao unachukulia shambulio lolote dhidi ya taifa mojawapo kama shambulio dhidi ya mataifa yote mawili.

Saudi Arabia 2025 | Mohammed bin Salman na Shehbaz Sharif
Saudi Arabia na Pakistan zimesaini mkataba wa ulinzi wa pamoja.Picha: Saudi Press Agency/REUTERS

Makubaliano haya muhimu yamefikiwa kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Qatar wiki iliyopita. Ufalme wa Saudi Arabia kwa muda mrefu umekuwa na uhusiano wa karibu wa kiuchumi, kidini na kiusalama na Pakistan, ikiwa ni pamoja na kuripotiwa kufadhili mpango wa silaha za nyuklia wa Islamabad wakati ulipokuwa ukitengenezwa.

Hata hivyo, muda wa kusainiwa kwa mkataba huu unaonekana kuwa ujumbe kwa Israel, ambayo kwa muda mrefu imeshukiwa kuwa taifa pekee la Mashariki ya Kati lenye silaha za nyuklia, na ambalo limeendesha mashambulizi makubwa ya kijeshi tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023, likizihusisha Iran, Lebanon, Mamlaka ya Palestina, Qatar, Syria na Yemen.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW