1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Pakistan: Mtu mmoja auawa akishutumiwa kuinajisi Quran

11 Februari 2023

Mamia ya Waislamu wamekishambulia kituo kimoja cha polisi katika mkoa wa Punjab mashariki mwa Pakistan na kumchukua mtuhumiwa anayedaiwa kutenda kufuru na kisha kumuua.

Selbstmordattentat Quetta / Pakistan / 05.2.23
Picha: Ghani Kakar/DW

Afisa mkuu wa polisi Babar Sarfaraz Alpa amesema mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina moja la Waris alikuwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kunajisi kurasa za kitabu kitakatifu cha Uislamu, Quran.

 Mashtaka ya kukufuru yanaadhibiwa kwa hukumu ya kifo chini ya sheria ya Pakistan. Mnamo Desemba 2021, kundi la watu lilimuua raia wa Sri-Lanka ambaye alikuwa meneja wa kiwanda cha vifaa vya michezo huko Punjab, kwa tuhuma za kukufuru.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW