1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Imran Khan awekewa kizuizi cha kusafiri nje ya nchi

26 Mei 2023

Serikali ya Pakistan imemuwekea kizuizi cha kusafiri waziri mkuu wa zamani Imran Khan. Kulingana na maafisa hao, mkewe Khan, Bushra Bibi na mamia ya wasaidizi wake wa kisiasa pia wamezuiwa kusafiri kwenda nje ya nchi.

Pakistan Ministerpräsident Imran Khan
Picha: K. M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Khan kupitia ukurasa wake wa Twitter ameikaribisha hatua hiyo ya kumuweka katika kile kinachojulikana kama Orodha ya Udhibiti wa Kuondoka, ECL, akisema hana mpango wa kwenda nje ya nchi, zaidi ya kuchukua likizo za mapumziko za nchini humo.  

Khan aliyeondolewa madarakani kwa kura ya bunge ya kutokuwa na imani mwaka uliopita, anakabiliwa na kesi kadhaa za ufisadi na hatua ya kukamatwa ya Mei 9 na kufikishwa mahakamani ilichochea maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 9 na baada ya siku tatu aliachiwa kwa dhamana na mahakama ya juu zaidi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW