1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yahitaji misaada ya dharura

20 Agosti 2010

Katika kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa siku ya Alkhamisi mjini New York, nchi kadhaa zimeahidi kutoa misaada zaidi kwa wahanga wa mafuriko nchini Pakistan.

United Nations Secretary-General Ban Ki-moon addresses the United Nations General Assembly, Thursday, Aug. 19, 2010, at United Nations headquarters. (AP Photo/Mary Altaff
Katibu Mkuu Ban Ki-moon akihotubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Picha: AP

Katika kikao hicho,Umoja wa Mataifa uliomba msaada wa dharura wa dola milioni 460. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon,akiwahimiza wanachama waliohudhuria kikao hicho cha dharura kutoa msaada zaidi alisema:

"Pakistan inakabiliwa na Tsunami inayoijongelea na kila wakati ukipita ndio maafa yake yatakapozidi kuwa makubwa."

Akasisitiza kuwa umoja huo unahitaji kwa dharura msaada wa dola milioni 460. Nusu ya fedha hizo zimeshaahidiwa, lakini ahadi zinapaswa kutimizwa kwa vitendo. Fedha zilizopokewa ni zaidi ya asilimia 60 ya zile zilizoahidiwa lakini fedha zote zinahitijiwa hivi sasa. Kwani kwa mujibu wa tarakimu mpya, jumla ya watu milioni 20 wameathirika kwa mafuriko hayo nchini Pakistan na watu milioni 8 wanahitaji msaada wa haraka. Idadi hiyo ni zaidi ya wale walioathirika kwa jumla katika maafa ya Tsunami, matetemeko ya ardhi yaliyotokea Kashmir na Haiti na kimbunga nchini Burma.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan,Shah Mahmood Qureshi.Picha: AP

Hata Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi alisisitiza:

"Kiwango cha maafa hayo ni changamoto kubwa mno kwa nchi yo yote ile inayoendelea kukabiliana nayo peke yake. Ni matumaini yetu kuwa jumuiya ya kimataifa itatusaidia kwa dhati."

Wakati wa kikao cha hiyo jana mjini New York mataifa mengi yaliahidi kutoa misaada mbali mbali-kuanzia matibabu hadi usafiri. Kwa mfano, kuna uhaba wa helikopta na hiyo ndio njia pekee ya kufikia maeneo yaliyofurika.

Waziri wa Nje wa Marekani, Hillary Clinton akiitikia mwito wa Katibu Mkuu Ban, aliahidi msaada mwingine wa dola milioni 60 na hivyo kufikia jumla ya dola milioni 150. Msaada huo utachangia kuipa Marekani sura nyingine katika nchi ambako inazidi kutazamwa kama ni dola kuu la kigeni lisiloeleweka.

Nchi zilizoahidi kutoa msaada zaidi ni Ujerumani itakayoongeza msaada wake kwa euro milioni 10 zingine na hivyo kufikia jumla ya euro milioni 25. Uingereza nayo imeongeza maradufu msaada wake kufikia dola milioni 100; na Umoja wa Ulaya hadi dola milioni 135. Kikao hicho cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitaendelea hii leo mjini New York na hapo ndio itakapojulikana iwapo umoja huo umefanikiwa kupata kiwango cha dola milioni 460 kilichoombwa na Katibu Mkuu Ban ki-Moon.

Mwandishi:Bodewein,Lena/ZPR

Mhariri:Charo,Josephat

MOD:

Katika kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa siku ya Alkhamisi mjini New York, nchi kadhaa zimeahidi kutoa msaada zaidi kwa wahanga wa mafuriko nchini Pakistan.Umoja wa Mataifa umeomba msaada wa dharura wa dola milioni 460. Zaidi anaeleza mwandishi wetu Lena Bodewein katika ripoti inayosomwa studioni na Prema Martin.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwahimiza wanachama waliohudhuria kikao hicho cha dharura kutoa msaada zaidi alisema:

CLIP BAN:

"Pakistan inakabiliwa na Tsunami inayoijongelea na kila wakati ukipita maafa yake yatazidi kuwa makubwa."

Akasisitiza kuwa umoja huo unahitaji kwa dharura msaada wa dola milioni 460. Nusu ya fedha hizo zimeshaahidiwa, lakini zinapaswa kutimizwa kwa vitendo. Fedha zilizopokewa ni zaidi ya asilimia 60 ya zile zilizoahidiwa lakini fedha zote zinahitijiwa hivi sasa. Kwani kwa mujibu wa tarakimu mpya, jumla ya watu milioni 20 wameathirika kwa mafuriko hayo nchini Pakistan na watu milioni 8 wanahitaji msaada wa haraka. Idadi hiyo ni zaidi ya wale walioathirika kwa jumla katika maafa ya Tsunami, matetemeko ya ardhi yaliyotokea Kashmir na Haiti na kimbunga nchini Burma.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mahmood Qureishi alisisitiza:

CLIP: QURESHI:

"Kiwango cha maafa hayo ni changamoto kubwa mno kwa nchi yo yote ile inayoendelea kukabiliana nayo peke yake. Ni matumaini yetu kuwa jumuiya ya kimataifa itatusaidia kwa dhati."

Wakati wa kikao cha hiyo jana mjini New York mataifa mengi yaliahidi kutoa misaada mbali mbali-kuanzia matibabu hadi usafiri. Kwa mfano, kuna uhaba wa helikopta na hiyo ndio njia pekee ya kufikia maeneo yaliyofurika.

Waziri wa Nje wa Marekani, Hillary Clinton akiitikia mwito wa Katibu Mkuu Ban, aliahidi msaada mwingine wa dola milioni 60 na hivyo kufikia jumla ya dola milioni 150. Msaada huo utachangia kuipa Marekani sura nyingine katika nchi ambako inazidi kutazamwa kama ni dola kuu la kigeni lisiloeleweka.

Miongoni mwa nchi zilizoahidi kutoa msaada zaidi ni Ujerumani itakayoongeza msaada wake kwa euro milioni 10 zingine na hivyo kufikia jumla ya euro milioni 25. Uingereza nayo imeongeza maradufu msaada wake kufikia dola milioni 100; na Umoja wa Ulaya hadi dola milioni 135. Kikao hicho cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitaendelea hii leo mjini New York na hapo ndio itakapojulikana iwapo umoja huo umefanikiwa kupata kiwango cha dola milioni 460 kilichoombwa na Katibu Mkuu Ban ki-Moon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW