1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yapendekeza duru ya pili ya mazungumzo

14 Aprili 2026

Marekani imeweka mzingiro katika bandari za Iran kuzuia meli, wakati Pakistan ikipendekeza mazungumzo mengine kumaliza vita vinavyoendelea

Pakistan imekuwa ikisimamia mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Marekani na Iran baada ya kuzuka vita Februari 28 vilivyoanzishwa na Marekani na Israel
Pakistan imekuwa ikisimamia mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Marekani na Iran baada ya kuzuka vita Februari 28 vilivyoanzishwa na Marekani na IsraelPicha: Anjum Naveed/AP Photo/dpa/picture alliance

Maafisa wa Pakistan wamefahamisha kwamba nchi hiyo imependekeza duru ya pili ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kumaliza vita inayoendelea.

Pendekezo la Islamabad limetolewa wakati Marekani ikiweka vizuizi kamili leo katika bandari za Iran, huku Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akisema mazungumzo na Iran yamepiga hatua na Rais Donald Trump akionesha jana Jumatatu kwamba Iran iko tayari kufikia makubaliano.

Pakistan yapendekeza awamu nyingine ya majadiliano ya usuluhishi kati ya Iran na Marekani

Kwa upande mwingine, jana afisa mmoja mwandamizi wa kundi la Hezbollah alisema kundi hilo halitozingatia makubaliano ya aina yoyote ambayo yatatokana na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel yatakayoanza leo huko Washington.

Maafisa wa serikali ya Lebanon wanatarajia kufikia makubaliano ya usitishaji vita katika mgogoro kati ya Israel na Hezbollah uliosababisha vifo vya takriban watu 2,089 nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW