1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroPakistan

Pakistan yatishia hatua za kijeshi dhidi ya Houthi wa Yemen

22 Julai 2026

Pakistan imetishia kuchukua hatua za kijeshi wakati mvutano ukiongezeka tena kati ya Saudi Arabia na waasi wa Houthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran.

Falme za Kiarabu Khor Fakkan 2026 | Meli za mizigo mbele ya bandari ya kontena kwenye Ghuba ya Oman
Pakistan imetishia kujibu mashambulizi ya Houthi wa Yemen waliotangaza mzingiro wa meli za Saudi ArabiaPicha: AFP

Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imeonya kwenye taarifa kwamba kitendo chochote cha uhasama dhidi ya meli zenye bendera ya Pakistan ama maslahi ya Pakistan baharini kitachukuliwa kuwa kitisho kikubwa kwa usalama wa taifa na maslahi yake ya kiutawala.

Pakistan yenye silaha za nyuklia ina ushirikiano mpana wa kijeshi na Saudi Arabia.

Waasi wa Houthi siku ya Jumatatu walitangaza mzingiro dhidi ya meli zinazohusishwa na Saudi Arabia, takriban wiki moja tangu kuzuka kwa mzozo mpya na taifa hilo jirani, ambalo limekuwa vitani na kundi hilo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW