1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan yatafakari kukipiga marufuku chama cha Imran Khan

24 Mei 2023

Pakistan inafikiria kukipiga marufuku chama cha waziri mkuu wa zamani Imran Khan, amesema waziri wa ulinzi, uamuzi ambao una uwezakano mkubwa wa kuwakasirisha wafuasi wake na kuchochea makabiliano zaidi na jeshi.

Pakistan Lahore | Ehemaliger Premierminister Imran Khan im AFP-Interview
Picha: Arif Ali/AFP/Getty Images

Nyota huyo wa zamani wa mchezo wa Kriketiameingia katika awamu ya karibuni zaidi na muhimu ya uhasama wa miongo kadhaa kati ya wanasiasa wa kiraia na jeshi lenye nguvu, ambalo limetawala moja kwa moja au kusimamia serikali katika historia yote ya Pakistan.

Mzozo huo umesababisha maandamano makubwa ya wafuasi wa Khan, na kuibua hofu mpya kuhusu uthabiti wa nchi hiyo yenye silaha za nyuklia wakati ikikabiliwa pia na mzozo wake mbaya zaidi wa kiuchumi katika miongo kadhaa.

Soma pia:Kashmir: Khan aapa 'kupambana hadi mwisho' 

Waziri wa Ulinzi Khawaja Asif amewaambia waandishi habari kwamba chama cha Khan cha Pakistan Tahreek-e-Insaf, OTI kimeshambulia misingi yote ya taifa, hali ambayo amaesema haiwezi kuvumiliwa, na kuongeza kuwa suala la kukipiga marufuku linazingatiwa ikiwa bunge litatoa idhini yake ya mwisho.

Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan akiondoka baada ya kuhudhuria mahakamani mjini Lahore, Pakistan, Mei 19, 2023.Picha: K. M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Waziri huyo alizungumzia maandamano ya wafuasi wa Khan ambao mwezi huu walishambulia miundombinu a jeshi, yakiwemo makao makuu ya jeshi hilo pamoja na majengo ya serikali.

Wakili wa chama cha PTI Ali Zafar amesema hatua kama hoyo itapingwa mahakamani, na kuongeza kuwa chama kizima hakiwezi kulaumiwa kwa vitendo vya watu binafsi.

Kukosana na jeshi na kuondolewa uongozini

Khan alichaguliwa waziri mkuu mnamo mwaka 2018 kwa kuungwa mkono na jeshi, ingawa pande zote mbili zilikanusha hilo wakati huo. Jeshi lilimuona Khan, pamoja na ajenda yake ya kihafidhina na kizalendo, kama mwenye uwezekano wa kuhakikisha ulinzi wa maslahi yake.

Soma pia: Wafuasi wa serikali Pakistan waandamana kumshinikiza jaji mkuu ajiuzulu

Lakini baadae Khan alikosana na majenerali baada ya kuonekana kama anaingilia upandishaji vyeo muhimu katika sekta ya usalama, na aliondolewa katika wadhifa wa waziri mkuu baada ya kupoteza kura ya imani bungeni.

Imran Khan ana kiu ya kukomesha machafuko Pakistan

00:47

This browser does not support the video element.

Tangu wakati huo, Khan mwenye umri wa miaka 70 amekuwa akiendesha kampeni ya kuitishwa kwa uchaguzi mkuu wa mapema, akiwahamasisha wafuasi wake kote nchini humo.

Lakini waziri mkuu aliechukuwa nafasi yake, Shahbaz Sharif, amekatiaa miito ya kufanyika uchaguzi kabla ya ule uliopanga baadae mwaka huu. Khan anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi ambayo ameyatupilia mbali akiyataja kuwa yamepikwa kujaribi kumzuwia kushiriki siasa.

Mnano Mei 9, waziri mkuu huyo wa zamani aliwekwa kizuwizini kuhusiana na mashtaka hayo, hatua iliyozusha maandamano ya wafuasi wake na mashambulizi yao dhidi ya vituo vya jeshi, kabla ya kuwaachiwa kwa dhamana baadae.

Wachunguzi wa mamlaka ya kupambana na rushwa walimhoji  hapo jana kwa karibu masaa matatu.

Chanzo: rtre

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW