1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yatoa wito wa kupanuliwa mpango wa BRI wa China

Sylvia Mwehozi
17 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ametoa wito wa kutanuliwa kwa mpango wa ujenzi wa miundombinu wa China BRI ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO
Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO Picha: Press Information Department via AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ametoa wito wa kutanuliwa kwa mpango wa ujenzi wa miundombinu wa China BRI ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda. Shehbaz ameyasema hayo katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO uliofanyika katika mji mkuu wa Pakistan wa Islamabad.

Kiongozi huyo alikuwa akihutubiamkutano wa wakuu wa serikali wa Jumuiya ya SCO,iliyoundwa mwaka 2001, na kuhudhuriwa na maafisa kutoka nchi 11, ikiwa ni pamoja na mwenyeji Pakistan, China, Urusi na India.

China ilizindua mpango huo wa dola trilioni 1 wa miundombinu ya kimataifa na mitandao ya nishati miaka kumi iliyopita ili kuunganisha Asia na Afrika na Ulaya kupitia njia za ardhini na baharini. Zaidi ya nchi 150, ikiwa ni pamoja na Urusi, zimejiandikisha kushiriki katika mpango huo tangu uzinduzi wake.