1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Pakistan yawakamata watu 10 kwa kuuza binadamu

18 Juni 2023

Mamlaka nchini Pakistan zimewakamata watu 10 wanaodaiwa kufanya biashara haramu ya binaadamu siku chache baada ya boti iliyokuwa imefurika wahamiaji kuzama karibu na pwani ya Ugiriki, maafisa wamesema.

Pakistan Shehbaz Sharif
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Mamlaka nchini Pakistan zimewakamata watu 10 wanaodaiwa kufanya biashara haramu ya binaadamu siku chache baada ya boti iliyokuwa imefurika wahamiaji kuzama karibu na pwani ya Ugiriki, maafisa wamesema.

Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif aidha ameagiza hatua kali na za haraka kuchukuliwa dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo akisema wataadhibiwa vikali.

Huenda kuna na idadi kubwa ya raia wa Pakistan miongoni mwa waliokuwa ndani ya boti hiyo kuukuu iliyozama siku ya Jumatano na kuua takriban watu 78 huku mamia wengine wakiwa hawajapatikana.

Kila mwaka maelfu ya vijana wa Paskistan hujaribu kuingia Ulaya kinyume cha sheria wakitumia njia za hatari, ili kutafuta maisha bora.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW