1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PALERMO:Wakimbizi wakamatwa karibu na Lampedusa

23 Oktoba 2005

Polisi nchini Italia wamewakamata wakimbizi 25 waliokuwa katika boti karibu na kisiwa cha Lampedusa.Wakimbizi hao,wengi wakiwa ni wanawake na akiwemo pia mtoto mmoja mchanga,wamepelekwa katika kambi maalum.Kwa mujibu wa polisi, wakimbizi hao ni Wasomali.Wakimbizi wanaotaka kukimbilia nchi za Umoja wa Ulaya hujaribu kwenda Italia kupitia kisiwa cha Lampedusa kilicho umbali wa kilomita 100 kutoka Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW