1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Palestina yaitaka jamii ya kimataifa kuitia kishindo Israel

15 Januari 2025

Mohammed Mustafa amesema usitishaji vita ni muhimu lakini hautoshim, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuishurutisha Israel kuheshimu sheria za kimataifa na kukubali suluhisho la mataifa mawili.

Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas
Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud AbbasPicha: Ayman Nobani/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina, Mohammed Mustafa, amesema Jumuiya ya Kimataifa italazimika kuendelea kuishinikiza Israel baada ya kufikiwa makubaliano ya amani Gaza, ikubali kuundwa kwa dola la Wapalestina.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa tatu wa muungano wa kimataifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa kuundwa madola mawili Mashariki ya Kati, waziri mkuu huyo wa Palestina, amesema Israel inapaswa kuoneshwa kipi ni haki na kipi ni makosa.

Soma pia: Baerbock afanya mazungumzo na maafisa wa Israel, Ukingo wa Magharibi

Amewaambia waandishi wa habari mjini Oslo kwamba kutumiwa kwa kura ya turufu katika kuzuia amani na uundwaji wa dola la Wapalestina ni jambo ambalo haliwezi kukubalika tena. Wajumbe kutoka takriban mataifa 80 na mashirika wamekutana Oslo, Norway katika mkutano huo wa Kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW