1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Josep Borrell azungumzia kuanzishwa taifa la Palestina.

21 Novemba 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kuanzishwa kwa taifa la Palestina kutakuwa njia bora zaidi ya kuhakikisha usalama wa Israel.

Besuch von EU-Außenbeauftragtem Josep Borrell und Israels Außenminister Eli Cohen in Kibbutz Beeri
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Borrell amefanya mkutano kwa njia ya video na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya baada ya kuizuru Mashariki ya Kati kwa mazungumzo juu ya mzozo kati ya Israel na kundi la Hamas.Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa, amepata kile alichokiita "hitimisho la msingi la kisiasa" kufuatia mazungumzo yake katika eneo la Mashariki ya Kati. Amesisitiza kuwa, Israel haifai kuchukua udhibiti wa Gaza baada ya mzozo wa sasa kumalizika na kwamba udhibiti wa eneo hili unapaswa kuwa mikononi mwa mamlaka ya Palestina.

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW