Pamba Jiji: "Tuko tayari kukabiliana na Yanga"
22 Septemba 2025
Pamba Jiji, wanatamba kuwa wako tayari kukabiliana na Yanga kama anavyozungumza afisa habari Moses William.
''Tumafahamu na tunatambua Mechi haiwezi kuwa nyepesi hata kidogo hatuendi kinyonge hata kidogo kwenye huu mchezo dhidi ya Yanga tunaenda kucheza na Timu kubwa ila Pamba Jiji ya Msimu huu sio wanyonge hata kidogo "Amesema afisa habari wa Pamba Jiji Moses William.
Wakati huo huo Simba Septemba 25 itakuwa Dimbani kupepetana na Fountain Gate katika Mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
"Hali ya wachezaji ni nzuri kabisa wachezaji wapo vizuri tupo tayari kwa maandalizi kwa ajili ya mechi yetu ijayo ambao utakuwa mchezo wetu wa klwanza kabisa kwa mechi ya Ligi ya NBC"Amesema Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola .
Tetesi za kocha Fadlu kutimkia Morocco
Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara bado iko katika hatua za mwanzo, mjadala mkubwa unaotikisa mitandao ya kijamii na vijiwe vya soka ni tetesi za kuondoka kwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davis kutimkia Morocco katika Timu ya Raja Casablanca licha ya kuwa bado hakuna tamko rasmi kutoka simba wala kocha mwenyewe, tetesi hizi zimeibua maswali mengi kuhusu mustakabali wa Timu hiyo kubwa nchini.
Iwapo ni kweli kocha Fadlu Davis ataondoka, basi swali kubwa ni je, huu ni wakati sahihi? Simba ipo kwenye maandalizi makali ya ligi na pia mashindano ya kimataifa Kuondoka kwa kocha katika kipindi hiki kunaweza kuvuruga mpangilio wa kikosi, hasa kwa wachezaji wapya waliowasajiliwa wakiwa na matumaini ya kufundishwa na kocha Fadlu Davis na Huu ni mtazamo wa wadau wa Soka.
''Kama itakuwa kweli basi kutakuwa na shida kwa sababu mwalimu alihitajika Tangu msimu wa Mwaka jana kwa hiyo ina maana yeye alitaka kututia sisi chaka atusajilie wachezaji halafu badaae aondoke"Amesema Mdau wa Soka
''Mwalimu unaondoka wakati Ligi kuu soka Tanzania Bara imeanza na Ligi ya Mabingwa Africa tunaweza tukasema ni pigo kwa Klabu ya Simba"Amesema Mdau wa Soka Lai Saidi
''Kwangu mimi naona inaweza isiwaathiri sana simba inawezekana anayekuja akaanzia pale mwenzake alipoishia na akaiendeleza tu Timu ikawa Bora ''Amesema Mdau wa Soka Ibrahim Jamal
Tetesi za kuondoka kwa Fadlu Davis bado hazijwekwa wazi, "Kuhusiana na mustakabali wa kocha Fadlu Davis klabu itatoa taarifa pale mambo yote yatakapokuwa yamekamilika wana simba tuwe watulivu tuendelee kuipambania simba yetu wanasimba hawapaswi kupaniki wala kuwa na unyonge"Amesema Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally
Jana kikosi cha Simba kimewasili Tanzania kikitokea Nchini Botswana na Kocha Msaidizi pekee Selemani Matola bila ya Kocha Mkuu Fadlu Davis na Kuendelea kuibua maswali mengi kwa Mashabiki.
//Mhindi Joseph