SiasaVenezuela
Panama yautambua ushindi wa upinzani huko Venezuela
3 Agosti 2024Matangazo
Rais Jose Raul Mulino ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X kwamba Panama inaungana na mataifa mengine kumtambua Gonzalez kama rais aliyechaguliwa wa Venezuela, na kusisitiza kuwa kuheshimu matakwa ya raia ndio msingi wa demokrasia.
Marekani pia ilitangaza wiki hii kumtambua Gonzalez kama mshindi wa uchaguzi huo. Upinzani na wananchi wanapinga matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi na yaliyompa ushindi rais Maduro.
Soma pia: Upinzani Venezuela kuandamana kupinga ushindi wa Maduro
Siku ya Ijumaa, majambazi waliofunika nyuso zao walivamia ofisi za chama cha upinzani, siku moja baada ya kiongozi mkuu wa upinzani Maria Corina Machado kusema anaishi kwa sasa mafichoni akihofia kuhusu uhai wake.