SiasaSudan
Pande hasimu Sudan kuanza tena mazungumzo Jumapili
13 Mei 2023Matangazo
Hayo yameelezwa Jumamosi na afisa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo, pande hizo zitaendelea kubaki kwenye mji wa Jeddah, Saudi Arabia ili kuanza duru ijayo ya mazungumzo baada ya kukubaliana siku ya Alhamisi kuhusu mpango wa kuwalinda raia.
Saudi Arabia pia imemualika Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan, katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League ambao umepangwa kufanyika mjini Jeddah Mei 19.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema kuwa takribani watu 200,000 wameyakimbia mapigano ya Sudan, wakiwemo watoto wengi wenye utapiamlo wanaowasili Chad.