1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Pande hasimu Sudan kurejea kwenye meza ya mazungumzo

7 Juni 2023

Pande hasimu zinazowania madaraka nchini Sudan zimekubaliana kurejea kwenye meza ya mazungumzo chini ya upatanishi wa Marekani na Saudi Arabia katika wakati mapigano bado yanaripotiwa kwenye mji mkuu Khartoum.

Themenpaket - Sudan
Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel-Fattah BurhanPicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Kituo cha Televisheni nchini Saudi Arabia cha Al-Arabiya kimeripoti kwamba jeshi la taifa na kikosi cha wanamgambo wenye nguvu wa RSF wamekubaliana kuanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuutafutia suluhu mzozo unaoendelea.

Hakuna maelezo ya ziada yaliyotolewa kuhusu habari hizo na pande hasimu nchini Sudan bado hazijatoa tamko lolote.

Licha ya taarifa hizo, mapigano bado yameutikisa mji mkuu wa Khartoum na viunga jirani usiku wa kumakia leo kwa mashambulizi ya anga na makabiliano ya ardhini.

Saudi Arabia na Marekani zimekuwa wapatanishi wa mzozo huo tangu ulipozuka kiasi miezi miwili iliyopita lakini bado hakuna usitishaji kamili wa mapigano ulioafikiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW