1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande mbili zinazozozana Yemen zaanza mazungumzo

11 Machi 2023

Umoja wa Mataifa umesema kuwa pande mbili zinazozozana nchini Yemen zimeanza mazungumzo kuhusiana na utekelezwaji wa mkataba iliousimamia kuhusu ubadilishanaji wa wafungwa.

Symbolbild Kämpfe im Jemen
Picha: AP Photo/picture alliance

Mazungumzo hayo kati ya serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na waasi wa Houthi yanafanyika nchini Uswisi na kusimamiwa kwa pamoja na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Hans Grundberg na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu

Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, Grundberg amezihimiza pande hizo mbili kushiriki kwa umakini katika mazungumzo hayo ili kuwaachia huru wafungwa wengi iwezekanavyo. Grundberg pia amezihimiza pande hizo mbili kutimiza ahadi zilizowekwa sio tu kati yao lakini pia kwa maelfu ya familia za Yemen ambazo zimesubiri kwa muda mrefu kuunganishwa tena.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW