1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa azuru Cameroon na ujumbe wa amani kwa eneo la migogoro

Josephat Charo
15 Aprili 2026

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ameondoka Algeria leo Jumatano akielekea Cameroon kwa ziara ya siku nne.

Papa Leo XIV ameondoka Algeria Jumatano akielekea Cameroon kwa ziara ya siku nne
Papa Leo XIV ameondoka Algeria Jumatano akielekea Cameroon kwa ziara ya siku nnePicha: Isabella Bonotto/Anadolu/picture alliance

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ameondoka Algeria leo Jumatano akielekea Cameroon kwa ziara ya siku nne ambayo inajumuisha ziara katika kitovu cha mzozo wa kujitenga wa karibu muongo mmoja, ambako anatarajiwa kuleta ujumbe wa amani.

Baada ya ziara yake ya kihistoria nchini Algeria, iliyogubikwa na mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga na ugomvi na Rais wa Marekani Donald Trump, Papa huyo anatarajiwa kuwasili baadaye katika eneo la Cameroon kunakozungumzwa Kifaransa, ambalo limekuwa likitawaliwa na Rais Paul Biya tangu 1982.

Papa Leo anatarajiwa kukutana na Rais Biya mwenye umri wa miaka 93 baadaye Jumatano katika mkutano ambao umewagawanya Wakatoliki nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW