1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa afuta ratiba zake za kazi kufuatia maumivu ya goti

26 Aprili 2022

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amelazimika kufuta ratiba ya kazi zake kwa mara ya pili mnamo muda usiozidi wiki moja.

Vatikanstadt | Ostermesse Papst Franziskus - "Urbi et Orbi"
Picha: YARA NARDI/REUTERS

Hali hiyo imesababishwa na maumivu ya goti ya mara kwa mara. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake iliyo katika makao makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican, Papa Francis amevunja shughuli zake zote za leo, ikiwa pamoja na kushiriki kwenye mkutano wa Baraza la Makadinali.

Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 pia anasumbuliwa na maumivu ya nyonga yanayomfanya adhoofike.

Hata hivyo, anatarajiwa kufanya ziara katika nchi kadhaa baadaye mwaka huu, ikiwa pamoja na za barani Afrika ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW